Kocha Cedric Kaze na Nkane wazungimzia mechi ya kesho dhidi ya Kagera sugar

Kupata Kifurushi cha bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa kesho Jumanne katika uwanja wa Azam Complex, yamekamilika


Kaze amesema pamoja na muda wa maandalizi kuwa mdogo, ushiriki wao katika michuano mbalimbali uumewafanya kuwa tayari kucheza kila baada ya siku tatu


Kaze amesema anatambua mchezo dhidi ya Kagera Sugar utakuwa mgumu kwa kuzingatia ubora wa wapinzani wao


"Katika mechi ya kwanza tulicheza na Kagera Sugar kule Mwanza tukapata ushindi wa bao 1-0, walipata mkwaju wa penati lakini wakakosa. Nakumbuka ni moja ya mechi tulizopata usumbufu mkubwa. Hivyo tumejiandaa kikamilifu kuhakikisha changamoto hiyo haijirudii," alisema Kaze


Kaze amesema wanatarajia kuwa mabadiliko kidogo katika kikosi watakachotumia hapo kesho kulingana na utayari wa wachezaji


"Kwa sasa kikosi chetu kimeongezeka baada ya wachezaji waliokuwa majeruhi kurejea. Morrison (Bernard), Denis (Nkane) na hata David Bryson wote wamerejea"


"Morrison tutaendelea kumrejesha kikosini taratibu ili kuhakikisha hapati madhara, tukumbuke mechi yake ya mwisho ya ushindani kucheza ilikuwa Disemba 25 2022. Hivyo ni mchezaji muhimu lakini ataendelea kupewa nafasi kwa tahadhari," aliongeza Kaze


Nae winga Denis Nkane amesema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo huku wakitambua wanahitaji kutimiza malengo yao ya kutwaa ubingwa


"Sisi kama wachezaji tunajua umuhimu wa mechi ya kesho hasa katika kujihakikishia tunatimiza malengo yetu ya kuchukua ubingwa, tuna imani tutafanya vizuri na kupata point tatu dhidi ya Kagera Sugar," alisema Nkane

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post