Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Taarifa kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa KMC inaeleza kuwa “Bodi ya timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) baada ya kukaa kikao mapema leo asubuhi imeamua kuvunja benchi lote laufundi lililokuwa likiongozwa na kocha Thier Hitimana baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili kutokana na kutoridhsihwa na mwenendo wa timu kwa msimu huu” Hivi basi Uongozi umefikia makubaliano na kocha Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ ambaye atachukua timu akiwa na benchi lake la ufundi” imeeleza taarifa hiyo
Kwa msimu huu Kocha Thiery Hitimana ameiongoza KMC katika michezo 26 ambapo wamefanikiwa kukusanya jumla ya pointi 26 kwa wastani wa pointi moja kila mchezo wakifungwa michezo 12, wakipata sare michezo 8 huku wakiwa wameshinda michezo mitano pekee huku wakifunga jumla ya mabao 29 wakiwa wamefungwa mabao 22 na wakiwa nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ambapo kama wakiendelea na mwenendo huo wanaweza kucheza Play Off ya kuepuka na janga la kushuka daraja.
Post a Comment