Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Msemaji wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuna haja ya uongozi wa klabu hiyo kuachana na kesi ya kiungo wa timu hiyo, Feisal Salum 'Fei Toto' inayoendelea TFF kwani tayari wameshapata mchezaji anayeweza kufanya makubwa kama aliyokuwa akiyafanya mwamba huyo kutoka Visiwa vya Karafuu Zanzibar.
Kamwe ametoa kauli hiyo kufuatia beki wao wa kati, Bakari Nondo Mwamnyeto kutoa assists mbili kwa Fiston Mayele kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers United nchini nigeria wikiendi iliyopita.
"Mwamnyeto ametufikirisha viongozi wake tuendelee na kesi ya Fei Toto au tumbadilishe namba Nondo aje kuwa namba 10 tumalize hili Jambo. Maana yake tunaweza kuendelea na kesi kumbe tuna maestro midfielder mwingine kwenye timu yetu," amesema Ally Kamwe.
Fei Toto amepeleka barua TFF kuomba Mamlaka hiyo ivunje makataba wake na Yanga kwa madai kuwa amekuwa akinyanyaswa na klabu hiyo.
Yanga wakiwa na mtaji wa mabao 2-0, watarudiana na Rivers United keshokutwa Jumapili katika Dimba la Mkapa jijini Dar.
Post a Comment