Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Feisal Salum amelitaka Shirikisho la Soka TFF kuvunja mkataba wake na Young Africans baada ya kukwama mara mbili mfululizo mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, ambayo ilikiri kumtambua kama Mchezaji halali wa Young Africans.
Angetille ambaye ni Mwandishi wa Habari za Michezo Mwandamizi nchini Tanzania, ameibuka na andiko alilolichapisha katika Mitandao ya Kijamii akionesha kushangazwa na mvutano, ambao amedai hauna tija zaidi ya Mchezaji kutambua taratibu za kuvunja mkataba, na sio kuihusisha Taasisi ambayo haina uwezo huo.
Angetille ameandika: Mpira wetu unaenda siko. Mchezaji ana mkataba na klabu, halafu anaiomba taasisi nyingine ivunje huo mkataba! Logic inakataa kabisa.
Afadhali angetaja hayo manyanyaso, lakini inaonekana ni utashi tu wa kutaka kuondoka. Huu ni ubabaishaji. Mtu ambaye amechoshwa na ubabaishaji angeomba kuondoka na klabu ambayo inamtaka ingejitokeza kumalizana na muajiri wake.
Football ina kanuni tofauti na ajira nyingine ambazo unaweza kuvunja mkataba wakati wowote unapopata greener pasture. Hivi akivunja mkataba ndio ataanza kutafuta klabu inayomfaa?
Hizo ni sinema, Uaminifu na uadilifu wa mtu hupimwa katika mambo kama haya. Respect aliyoipata na vitu vinavyofanyika ni vitu viwili tofauti. Alishakuwa mchezaji mkubwa lakini anazidi kushusha hadhi yake. Kuaminika baadaye huko aendako itakuwa issue”
Post a Comment