Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wydad Casablanca kwenye mechi ya robo fainali ya mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Simba, Robertinho Oliveira, amesema kazi bado haijamalizika na wataenda na sura mpya katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Ijumaa nchini Morocco
Simba inatarajiwa kusafiri nchini Morocco kwa ajili ya mechi ya marudiano Aprili 28, mwaka huu katika Uwanja wa Mohammed V, kusaka ushindi ama sare yoyote ili kutinga nusu fainali
Robertinho amesema anatambua mchezo wa pili utakuwa tofauti hivyo ataandaa mkakati tofauti wa uchezaji ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ambayo yatawavusha hatua inayofuata
"Haitakuwa mechi rahisi na tutalazimika kucheza kwa mbinu tofauti, na wachezaji kuingia kivingine katika mchezo wa marudiano tofauti na tulivyocheza nyumbani ili kufikia malengo yetu ya kusonga mbele kucheza nusu fainali," alisema Robertinho
Robertinho amesema anaimani kubwa na wachezaji aliokuwa nao ndani ya kikosi kuwa watafanikisha malengo yao
Simba itacheza uwanja wa Mohammed V kwa mara ya pili msimu huu katika michuano ya ligi ya mabingwa
Mara ya mwisho walicheza na Raja Casablanca kwenye hatua ya makundi na kupoteza kwa kufungwa mabao 3-1
Post a Comment