Ishu ya Jean Baleke kurudi To mazembe Simba watoa maamuzi haya

Kupata Kifurushi cha bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Jean Baleke ameendelea kuwafunga mdomo waliokuwa wakimchukulia poa mara alipotua Simba kwenye dirisha dogo, baada ya jamaa kufunga jumla ya mabao 12 yakiwamo matano ya Ligi Kuu, manne ya Kombe la ASFC na matatu ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Kasi hiyo ya kufunga mabao imewafanya mabosi wa Simba kumzuia asirudi tena TP Mazembe ya DR Congo iliyowapa Msimbazi imtumie kwa kwa mkopo wa miezi sita, kwa kuanza mazungumzo ya kumpa mkataba ili asalie kikosini jumla na kuendelee kuwapa burudani na kuibeba timu hiyo.


Baleke alijiunga na Simba katika dirisha dogo la usajili lililofungwa Januari 15 mwaka huu na straika huyo Mkongoman mwenye umri wa miaka 21, sasa anaandaliwa mkataba mpya utakaomdhibiti kuondoka kikosini hapo hadi mwaka 2025.


Baleke alijiunga na Simba kwa mkataba uliokuwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja na nusu kama ataonyesha kiwango bora na sasa baada ya kufanya vizuri uongozi wa Simba umeanza kufanya marejeo 'review' ya mkataba huo ili kumbakiza jumla na kumuongezea baadhi ya maslahi.


Hali hiyo imekuja baada ya straika huyo kuwa na kasi ya kupachika mabao na kufikisha jumla ya mabao 12 ndani ya Simba  na kuisaidia kuipeleka timu hiyo robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la ASFC na kwenye ligi ipo nafasi ya pili nyuma ya Yanga.


Sambamba na hilo, Simba itampa mkataba huo Baleke kwa lengo la kumfunga kutoondoka kikosini hapo na kwenda katika timu nyingine ambazo zimeonyesha nia ya kumtaka ikiwemo TP Mazembe na Al Hilal ya Sudan.


Hata hivyo, tumepenyezewa taarifa na moja ya wasimamizi wa Baleke aliyeomba jina lake kuhifadhiwa kuwa kila kitu kiko tayari na siku sio nyingi Baleke atasaini mkataba huo.


"Mkataba wa mwanzo ulikuwa unahitaji review (marejeo) baada ya miezi sita kama atafanya vizuri, na sasa amefanya kile walichohitaji hivyo muda si mrefu atasaini tena mkataba wa uhakika utakaomuweka Simba hadi mwaka 2025," kilisema chanzo hicho na kuongeza;


"Mkataba huo utakuwa na mabadiliko kadhaa ikiwemo maslahi na kumfanya moja kwa moja awe mali ya Simba tofauti na ilivyokuwa awali."


Aidha msimamizi huyo alisema Baleke anafurahi kuwa Simba na anataka kuendelea kuonyesha ubora wake ndani akiwa ndani ya jezi nyekundu na nyeupe.


"Baleke ana furaha kuwa Simba, ana shauku ya kufanya makubwa akiwa na timu hiyo na kwa sasa hana malengo ya kuondoka hivyo mashabiki wake wasiwaze juu ya hilo." Kwa upande wa Simba, Mtendaji Mkuu wa klabu  hiyo, Imani Kajula aliliambia Mwanaspoti kuwa, hakuna mchezaji ambaye Simba inamhitaji atakayeondoka na zaidi watafanya maboresho ya mikataba yao.


"Hakuna mchezaji ambaye ataondoka Simba kama bado huduma yake inahitajika, tutakacho kifanya ni kuboresha baadhi ya mikataba ambayo inakaribia mwisho na mingine kutokana na makubaliano ya pande zote mbili yalivyo," alisema Kajula.


Wakati Baleke akiwa akijihakikishia maisha marefu ndani ya Simba, kwa upande wa nyota watatu wa kigeni, Augustine Okrah, Mohamed Ouattara, Peter Banda nafasi yao kusalia kwa msimu ujao ni finyu kutokana na kushindwa kumshawishi kocha Roberto Oliveira 'Robertinho' anayepanga kusajili mashine mpya katika maeneo yao mwishoni mwa msimu.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post