Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Wakati mkataba wake na Simba ukielekea ukingoni mwishoni mwa msimu, ni wazi 'legendary' huyu zama zake na Simba zinaelekea mwisho
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema Mkude yuko fit na anashiriki program za mazoezi Mo Simba Arena lakini amekuwa hachezi kutokana na sababu za kiufundi
Hajaweza kumshawishi Kocha Robertinho Oliveira ambaye katika nafasi ya kiungo mkabaji huwatumia zaidi Mzamiru Yassin, Sadio Kanoute na Ismail Sawadogo ambaye hata hivyo nae amepoteza nafasi yake mapema tu tangu alipotua kwenye dirisha dogo
Mkude ndiye mchezaji aliyedumu zaidi kwenye kikosi cha Simba, yuko na wekundu wa Msimbazi kwa zaidi ya miaka 13
Post a Comment