Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amependekeza kurejeshwa kikosini kwa kiungo mshambuliaji Hassan Dilunga pale dirisha la usajili litakapofunguliwa
Mwaka mzima Dilunga alikuwa nje baada ya kuumia mazoezini, sasa ni miezi kadha imepita mchezaji huyo anafanya mazoezi na timu hiyo, jambo lililomshawishi Robertinho kukubali kiwango chake
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba zimebainisha kuwa Robertinho amewaambia viongozi kwamba ukianza usajili waanze na Dilunga anaona anamfaa kwenye kikosi chake
"Kwenye mazoezi Dilunga anaonyesha kiwango cha juu, kinachomfanya kocha aamini ni kati ya wazawa ambao wanaweza wakawa msaada mkubwa ndani ya kikosi chake msimu ujao"
"Dilunga aliumia akiwa na Simba, ndio maana alipewa nafasi ya kufanya mazoezi na wenzake, pamoja na hilo mchezaji mwenyewe hakujibweteka anapenda mazoezi na alionyesha ana kitu kikubwa kinachomfanya kocha apende kumuona kwenye kikosi chake na nafakiri ameshawaambia uongozi kuwa anamhitaji kwa ajili ya msimu ujao, kama watawezana basi ataonekana kwenye jezi ya Simba," alibainisha mtoa taarifa
Post a Comment