Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kaze amesema Yanga inakwenda katika mchezo huo ikiwa na kikosi chake kamili, ni mchezzaji mmoja tu, Aboutwalib Mshery ambaye ni majeruhi
"Tumejiandaa vizuri kwa mchezo huu mkubwa. Tunafurahi tunakwenda kwenye mchezo tukiwa na wachezaji wote isipokuwa mlinda lango Aboutwalib Mshery ambaye yuko anaendelea na matibabu"
"Hii ni mechi kubwa lengo letu ni kushinda. Wakati wa maandalizi tumefanya kila kitu muhimu kwa ajili ya mechi yenyewe kitu kikubwa ni kuwa na kiwango bora, tuweze kucheza vizuri na kupata matokeo mazuri"
"Umuhimu wa ushindi katika mchezo huu utatuweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa, hivyo hii ni motivation kubwa kwa wachezaji wetu," alisema Kaze
Kaze pia amesema kucheza na Simba kabla ya mchezo wa robo fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United ni kitu kizuri kwao kwani itawapa mwanga wa nini watapaswa kufanya katika mchezo huo
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, kiungo Mudathir Yahya amesema wachezaji wote wamejiandaa na mchezo huo na wako tayari kupambana
"Wachezaji wote tumejiandaa vyema kupigania alama tatu. Hakuna presha yoyote tumejipanga na tutapambania ushindi," alisema Mudathir
Post a Comment