Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mwamuzi kutoka Afrika Kusini Abongile Tom atachezesha mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Rivers United dhidi ya Yanga
Mchezo huo utapigwa Jumapili, April 23 katika uwanja wa Godswill Akpabio International Stadium
Waamuzi Wasaidizi ni Ivanildo Meirelles de Oliveira Sanches kutoka Angola na Abelmiro Dos Reis Monte Negro kutoka visiwa vya Sao Tome
Mwamuzi wa akiba ni Djindo Louis Houngnandande kutoka Benin wakati waamuzi wa VAR ni Hamza El Fariq na Adil Zourak wote kutoka nchini Morocco
Kikosi cha Yanga tayari kiko Nigeria kuelekea mchezo huo ambao Wananchi wanahitaji kushinda au hata matokeo ya sare ugenini
Post a Comment