Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally ametamba kuwa kwa namna yoyote ile, mtani wao Yanga SC lazima apigwe kwenye mechi yao ya Dabi.
Simba inatarajia kumkaribisha Yanga katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar ikiwa na kumbukumbu ya kutopata matokeo chanya kwa takriban miaka mitatu iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari, Ahmed Ally amesema, kama uongozi utafanya kila linalowezekana kufanyika ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mechi hiyo muhimu kwao.
"Haiwezekani unamfunga tu Horoya halafu kuna timu inayotoka hapa tu Jangwani ikisumbue, uongozi utafanya kila linalowezekana na mashabiki tunaomba sana wafanye lolote linalowezekana ili kwa pamoja tuweze kufurahia ushindi," alisema.
Simba anakwenda kwenye mechi hiyo ya 26 ya dabi akiwa nyuma kwa pointi 8 akiwa nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi zake 60 huku Yanga akiwa kileleni na alama zake 68.
Post a Comment