Habari za asubuhi Wananchi, asanteni kwa sapoti yenu ya jana (juzi), tumewaangusha na inauma sana" Musonda

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mshambuliaji wa Yanga SC, Kennedy Musonda amewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo kutokana na kipigo cha bao 2-0 kutoka kwa watani zao wa Jadi, Simba Sc uliopigwa juzi Aprili 16, 2023 katik dimba la Mkapa.


Musonda ambaye ni raia wa Zambia amewashukuru pia mashabiki wa klabu hiyo kwa kuendelea kuwasapoti huku akiahidi kuwa watarejea kwa nguvu na ari zaidi ili kutimiza malengo waliojiwekea katika msimu huu.


"Habari za asubuhi Wananchi, asanteni kwa sapoti yenu ya jana (juzi), tumewaangusha na inauma sana, imekuwa ngumu kuamka leo baada ya kupoteza dabi yangu ya kwanza lakini tunawahitaji mashabiki zetu sasa kuliko hapo awali.


"Tumejifunza kutokana na makosa yetu na tutarudi tukiwa na nguvu na njaa zaidi ya mafanikio," amesema Musonda.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post