Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mayele anaongoza mbio za kuwania ufungaji bora ligi kuu ya NBC akiwa na mabao 16, mabao sita zaidi ya Moses Phiri na Saido Ntibazonkiza wa Simba wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na mabao 10
Aidha katika michuano ya CAF CC, Mayele anaongoza pia akiwa amefunga mabao matano sawa na Ranga Chivaviro wa Malumo Ganants wote wakifunga mabao matano
Mayele ameweka wazi shauku yake ya kuwa mfungaji bora wa ligi na kombe la Shirikisho ili kupamba msimu wake bora zaidi katika maisha yake ya kusakata kabumbu
"Yatakuwa mafanikio makubwa kwangu kama nitafanikiwa kuwa mfungaji bora wa mashindano ya CAF. Nawashukuru wachezaji wenzangu, tunashirikiana vizuri kuhakikisha tunatimiza malengo ya timu, lakini kama itatokea nimekuwa mfungaji bora nitafurahi sana"
"Mwaka jana sikushinda ufungaji bora wa ligi lakini mwaka huu naona inawezekana bado kuna mechi zimebakia, naweza kufanikiwa," alisema Mayele
Msimu huu Mayele amepachika mabao 31 katika michuano yote na kufikisha mabao 50 tangu alipojiunga na Yanga mwaka 2021
Post a Comment