Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
"Unafikiri hayo yote yalitokea kwa bahati mbaya ? Si kweli. Siri nyuma yake ni kutopoteza FOCUS. FOCUS yetu ni nini msimu huu ? Kubeba Makombe"
"Kila mwanayanga anataka kuiona timu yake ikibeba kombe la ligi kuu, FA na Ubingwa wa Africa Tunaimaliza April. Mwezi unaofuata, In shaa Allah utakuwa mwezi wa mapigano makubwa katika kuyatimiza malengo yetu"
"Vyakula vyote vizuri bado viko juu ya meza yetu. Tutulie na tushikane Wananchi. Kupoteza pambano sio kupoteza vita. Jana tumepoteza pointi (3) hatujapoteza malengo yetu ya Ubingwa msimu huu"
"Ushindi wa Kolo naufananisha na ushindi wa mke wa Achraf Hakimi . Ameshinda kesi lakini mgao Nehi Hivyo Kolo yoyote akikupigia kelele leo, mwambie Wewe huna tofauti na mke wa Hakimi,, Blaa blaa nyingi lakini wako palepale "
"Yanga tuko TOP OF THE TABLE na tutakwenda kuzimalizia mehi (4) za mwisho kwa nguvu kubwa zaidi INSHAA ALLAH"
"Kituo kinachofuata tunakwenda Nigeria . Mnawajua Wachezaji wetu, hii itakuwa mechi kubwa ya wao kupambana kuhakikisha tunashinda Mchezo huo na kuwapelekea Wananchi nusu fainali"
Post a Comment