Dimba la Mkapa kufanyiwa marekebisho mwezi wa Tano

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Ally Mayay amesema Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es salaam utafungwa rasmi Mei, mwaka huu kupisha matengenezo makubwa ya takribani miezi miwili


Licha ya uwanja huo kuelezwa ulishaanza matengenezo madogo madogo huku ukiendelea kutumika kwa mechi kubwa, Mayay amesema kuwa utafungwa baada ya kuanza kwa matengenezo ya eneo la kuchezea.


Amesema matengenezo hayo ya eneo la kuchezea yatasimamiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika 'CAF' kutokana na uwepo wa michuano ya CAF Super Cup


"Sababu kilichokuwa kinafanyika sasa hivi ni matengenezo ya baadhi kama vyumba vya kubadili nguo, maeneo ya wanahabari, vyumba vya waamuzi ambayo ni maboresho madogo lakini yale makubwa yataanza mwezi wa tano ambapo matumizi ya uwanja hayatakuwepo na inatarajia kuwa si chini ya wiki sita mpaka nane," amesema Mayay.


Amesema hayo ni marekebisho ya kawaida kama ilivyoelezwa hapo awali kwani kiwango na ubora wa uwanja hutengenezwa na kutumika kulingana na nyakati husika lakini muda unavyozidi kwenda, inapaswa kufanyiwa maboresho kuendana na nyakati


Kwa maelezo hayo, uwanja huo unaotumika kama uwanja wa nyumbani wa timu za Simba SC na Young Africans, unatarajiwa kutumika na timu hizo kwenye mechi za Robo Fainali za klabu Afrika kabla ya kuanza matengenezo ya eneo la kuchezea.


Na kwa mujibu wa ratiba ya Shirikisho la Soka la Barani Afrika 'CAF' ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mashindano hayo yanatarajiwa kufikia tamati Juni 11, 2023.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post