Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kiungo Mshambuaji wa Vinara wa Ligi Kuu ya England Arsenal Bukayo Saka amewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo, kufuatia kitendo cha kukosa Penati muhimu katika sare ya mabao 2-2, dhidi ya West Ham Utd.
Arsenal waliambulia sare hiyo wakicheza katika Uwanja wa ugenini jijini London Jumapili (April 16), wakitangulia kufunga mabao mawili, lakini baadae yalirudi na kuzifanya timu hizo kugawana alama.
Saka alitumia nafasi ya kuzungumza na vyombo vya habari baada ya mchezo huo, kuomba radhi kwa kitendo cha kukosa mkwaju wa Penati, ambao unaaminika kama angefanikiwa kuukwamisha wavuni, basi Arsenal ilikuwa ikiondoka na alama tatu.
“Kutokana na kilichotokea, siku zote nabeba majukumu, haijalishi nini kitatokea, nawaomba radhi mashabiki wa Arsenal, nitafanya juu chini kuweka mambo sawa,” amesema Saka
Huo ulikuwa mchezo wa pili mfululizo ambao Washika Bunduki wanadondosha alama, wakitangulia kupata sare ya 2-2 dhidi ya Liverpool, hali ambayo inaendelea kuwapa changamoto katika mbio za ubingwa dhidi ya Man City inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya alama nne.
Wakati huo huo Arsenal inakabiliwa na pigo kubwa baada ya kuripotiwa kwamba beki wao William Saliba hatakuwapo kwenye mchezo muhimu wa kutambua hatima yao kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu dhidi ya Manchester City.
Arsenal watakabiliana na wapinzani wao kwenye mbio hizo za ubingwa, Aprili 26 ugenini katika Uwanja wa Etihad.
Kwa mujibu wa Evening Standard Arsenal watakabiliana na Man City Ijumaa bila ya huduma ya Saliba.
Mchezaji huyo bado hajapona vyema majeruhi yake aliyopata kwenye mechi ya Europa League dhidi ya Sporting Lisbon ya Ureno.
Chanzo: Dar24
Post a Comment