Bondia Najum aliyeanguka ulingoni Dodoma afariki Dunia

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Najum kutoka jijini Mbeya amefariki Dunia mchana wa leo katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma (General) alipokuwa akipatiwa matibabu.


Najum alianguka ulingoni Jumapili iliyopita baada tu ya kumalizika kwa Pambano lake la raundi nne dhidi ya bondia wa Dodoma Laurent Segu, na kuwahishwa hospitali ambapo inaarifiwa alifanyiwa upasuaji mdogo wa kichwa hadi Asubuhi ya leo hali yake ilizidi kuimarika kabla ya kufikwa na mauti mchana wa leo.


Bondia huyo alikuwa amecheza mapambano matatu tu ya ngumi za kulipwa pamoja na hilo la Jumapili iliyopita, ambapo ameshinda Moja na kupoteza mawili.


Mwamuzi na Jaji wa kimataifa wa Tanzania, Pendo Njau ambaye alikuwa karibu na Bondia huyo amesema:"Ni kweli Ibrahim amefariki mchana wa leo saa sita alipokuwa amelazwa, nimepokea taarifa kutoka kwa Mama Sophia Mwakagenda ambaye ndiyo alikuwa promota.


"Sasa mwili ushatolewa hospitali wanaelekea Kyela Mbeya kwa ajili ya mazishi,"

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post