Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Baadhi ya wachambuzi na mashabiki wa soka nchini wamekuwa wakimsema kiungo wa Yanga raia wa Burkina Faso, Stephanie Aziz Ki kuwa hayupo kwenye kiwango kizuri kama alivyokuwa ASEC Mimosas ya Ivory Coast msimu uliopita.
Wengi wameenda mbali zaidi na kudai kuwa kwa usajili huo, Yanga wamepigwa, jambo ambalo limewaibua kundi la pili akiwemo msemaji wa klabu hiyo, Ally Kamwe wakimtetea na kusema kuwa zipo nyakati mchezaji anaweza kushuka lakini ukweli unabakia kuwa daraja lake na uwezo wake upo palepale.
Aziz Ki akiwa katika klabu ya ASEC Mimosas ambapo alikuwa mchezaji bora wa msimu ligi kuu ya Ivory Coast 2021/22 aliweka takwimu hizi katika mashindano yote ambayo klabu hiyo ilishiriki.
Mabao: 10 = Ligi kuu (7) + CAF (3)
Assist: 07 = Ligi kuu (5) + CAF (2)
Aziz Ki akiwa Yanga 2022/23
Mabao: 12 = Ligi kuu (8) + CAF (2) + FA (2)
Assist: 07 = Ligi kuu (3) + CAF (2) + FA (1) + (1) Ngao ya Jamii.
Huyu ni Mwamba wa Ouagadougou ambaye mpaka sasa amecheza mechi chache, ameanza mechi chache kuliko msimu uliopita akiwa ASEC na bado mashindano yanaendelea.
Takwimu hupingwa kwa takwimu, turudi kwenye hoja, wanaosema Aziz Ki yupo chini ya kiwango, hajaonyesha Wananchi walichokitarajia kutoka kwake, ni kipi hicho qmbacho walikiona ASEC na leo hajakifanya akiwa Yanga?
Dondosha comment yako!
Post a Comment