Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA
Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Gabriel Jesus alimaliza ukame wake wa mabao wa miezi sita akifunga mara mbili katika ushindi wa 4-1 wa Arsenal dhidi ya Leeds huko Emirates.
Mshambulizi huyo wa Brazil alikuwa anaanza kwa mara ya kwanza Ligi Kuu ya Uingereza 2023 baada ya kupona kutokana na upasuaji wa goti.
Akianza kikosini nafasi ya Bukayo Saka ambaye ni mgonjwa, Jesus alilipa imani ya Mikel Arteta kumwanzisha
Na ni mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aliyefungua ukurasa wa mabao kaskazini mwa London, huku Arsenal wakitangulia katika dakika ya 35
Jesus alishinda penalti baada ya kukatwa na beki wa kulia wa zamani wa akademi ya Gunners Luke Ayling na mwenyewe kufunga mkwaju huo wa penati
Lilikuwa ni bao lake la kwanza tangu kufunga katika ushindi wa 3-1 dhidi ya wapinzani wao Tottenham mnamo Oktoba 1 miezi sita iliyopita
Ben White akaiongezea Arsenal bao la pili kabla ya Jesus kuongeza jingine la tatu na Grait Xhaka kuhitimisha bao la nne. Bao pekee la kufutia machozi kwa Leeds lilifungwa na Rasmus Krintensen
Ushindi huo umerejesha gap la pointi baina yake na Manchester City kuwa nane, Arsenal ikiwa imecheza mechi moja zaidi
Post a Comment