Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Arsenal itakua mgeni wa Manchester City katika Uwanja wa Etihad baadae leo Jumatano, huku mchezo huo ukitazamwa kama hatma ya klabu hiyo ya jijini London, katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England.
Mwishoni mwa juma lililopita Arsenal ilikwama mbele ya Southampton baada ya kulazimishwa sare ya mabao 3-3 mchezo ambao ulipigwa Ijumaa (April 21).
Baada ya matokeo hayo, Arsenal imefikisha pointi 75 baada ya michezo 32 huku Man City wakiwa na alama 70 baada ya michezo 30 kwa maana hiyo wana viporo vya michezo miwili.
Kuelekea katika mchezo wa leo dhidi Manchester City, Meneja wa Arsenal Mikel Arteta amesema walifanya makosa katika mchezo uliopita dhidiya Southampton, lakini wachezaji wake walipambana na kuamka tena na anaamini wafanya vizuri leo katika Uwanja wa ugenini.
“Sitaki kusubiri kuna mechi nyingi ambazo tunatakiwa kucheza. Pale mambo yanapokuwa katika hali ngumu ndiyo wakati wa kupambana na kupata matokeo.”
“Tumejiandaa na tumejipanga kwa ajili ya mchezo ujao na hivi ndiyo soka lilivyo kuna wakati unahitaji kuwa katika nafasi fulani, ila mambo yanaenda tofauti. Lakini tumejiandaa kwa ajili ya kwenda kupambana kule Manchester, ” amesema Arteta.
Post a Comment