Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mchezo huo utapigwa kesho Jumapili, April 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari, Nabi alisema hakuna jambo wanahitaji zaidi ya kupata ushindi dhidi ya Rivers United na kusonga mbele hatua ya nusu fainali
Nabi amesema ushindi waliopata Nigeria hautakuwa na maana kama watakosa ushindi katika mchezo wa kesho utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
"Wachezaji wote wako vizuri, wanajituma sana mazoezini. Tunajua bado hatujafuzu, tunahitaji matokeo mazuri ili tusonge mbele hatua inaofuata"
"Nimekaa na wachezaji wangu, tumekubaliana kazi nzuri tuliyoifanya Nigeria itakuwa haina maana kama haitashinda mchezo wa kesho," alisema Nabi
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, kiungo Zawadi Mauya amesema wanafahamu ushindi katika mchezo huo utawafanya waandike historia ya kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza
"Tunajua tunakwenda katika mchezo ambao utaandika historia kwa klabu yetu. Lengo letu ni kuvuka ni kuvuka hapa na kufika mbali zaidi. Lakini kwa sasa tunaangalia mchezo uliopo mbele yetu tunahitaji ushindi tusonge mbele," alisema Mauya
Post a Comment