Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Daktari wa Kagera Sugar, Abel Shindika amesema mlinzi Datius Peter ambaye alikumbwa na changamoto ya kuzimia katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City, hakupata tatizo kubwa
Datius alizimia ghafla uwanjani baada ya kugongana na mshambuliaji wa Mbeya City, Sixtus Sabilo dakika ya 38 wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Aprili 23 kwenye Uwanja wa Kaitaba na wenyeji kushinda bao 1-0
Shindika amesema nyota huyo alipata mshtuko baada ya kugongwa sehemu ya goti lake kwa nyuma hivyo kumsababishia kupoteza fahamu ila baada ya kufanyiwa vipimo amegundulika hana tatizo lolote
"Tulimpima pale pale uwanjani lakini baada ya hapo tukampeleka hospitali ya karibu kwa ajili ya matibabu zaidi na tukagundua alipata mshtuko mdogo tu ambao hauna madhara yoyote hivyo anaendelea vizuri kwa sasa," alisema
Datius amesema lilikuwa jambo la kushtua katika maisha yake kwa sababu hali kama hiyo hajawahi kukutana nayo tangu ameanza mpira, hivyo anashukuru kwa sapoti kubwa ambayo wachezaji wenzake waliionyesha
"Nakumbuka nilizinduka hospitalini na baada tu ya hapo kitu cha kwanza niliuliza vipi matokeo, nikaambiwa tumeshinda basi kuanzia pale nikazidi kupata nguvu mwilini na nashukuru hadi sasa naendelea vizuri," alisema
Post a Comment