Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA
Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mlinzi wa kushoto wa Yanga Joyce Lomalisa ameendelea kuwa bora kutokana na kiwango bora anachoonyesha katika kikosi cha Yanga.
Kwa sasa unaweza kusema Lomalisa ndiye mchezaji mahiri zaidi upande wa kushoto katika ligi kuu ya NBC.
Lomalisa ametajwa kwenye kikosi cha wiki cha CAF kwa michuano ya kombe la Shirikisho sambamba na mshambuliaji Kennedy Musonda.
Mcongomani huyo pia alijumuishwa kwenye kikosi cha CAF cha Shirikisho baada ya mechi za raundi ya nne. Utofauti wa Lomalisa na walinzi wengi wa pembeni ni uwezo wake mkubwa wa kupanda na kushuka.
Ukiangalia mchezo uliopita dhidi ya US Monastir, Lomalisa ni kama alikuwa akicheza winga akimpa uhuru Kennedy Musonda kuingia ndani kuungana na Fiston Mayele pale timu inaposhambulia.
Lomalisa ndiye mchezaji aliyepiga krosi nyingi zaidi katika mchezo huo (7), takwimu zikimuonyesha kuwa mchezaji aliyehusika katika mashambulizi mengi ya Yanga.
Wakati mwingine Nabi anaweza kumtumia kama winga na huenda akawa na madhara zaidi akitumika katika nafasi hiyo kutokana na aina ya ucehzaji wake
Post a Comment