UONGOZI wa Klabu ya Yanga umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa timu ya Wanawake, Yanga Pirincess, Sebastian Nkoma.
Uamuzi huu umefikiwa baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
Uongozi wa Yanga umesema kuwa unamshukuru Kocha Sebastian kwa kazi yake kipindi chote alichokuwa akiifundisha timu yetu ya Wanawake.
Kutokana na hilo benchi la ufundi la Yanga Princess litakuwa chini ya kocha Fredy Mbuna mpaka mwisho wa msimu huu wa 2022/2023.
Post a Comment