Yanga ipo kileleni mwa Kundi D kwa faida ya magoli ikiwa na pointi 10 sawa na US Monastir, sasa inasaka rekodi ya kumaliza hatua ya makundi ikiwa nafasi hiyo ambayo ina faida ya kuanzia ugenini mchezo wa Robo Fainali na kumalizia nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar es salaam.
Kwenye mchezo huo wa Jumapili vs TP Mazembe, Yanga SC itahitaji ushindi mnono ambao utaifanya US Monastir itayocheza dhidi ya Real Bamako isiwfikie ili kujihakikishia nafasi hiyo ya Kwanza kwenye Kundi D.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa TP Mazembe Jijini Lubumbashi, DR Congo kuanzia Saa 10:00 Jioni.
Post a Comment