Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kwa sasa mashabiki wa Yanga wana raha ya aina yake baada ya kuishuhudia timu yao ikitinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Wananchi wanaona kabisa ni msimu ambao huenda wakaenda kushuhudia kupatikana mafanikio makubwa katika klabu yao kwenye miaka ya hivi karibuni
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema baada ya kufanikiwa kutinga robo fainali ya kombe la Shirikisho, malengo sasa ni kuitafuta nusu fainali, fainali na hata kusaka taji la kwanza barani Afrika kwani inawezekana
Wakati bendera ya Kimataifa ikiendelea kupepea vyema, Yanga pia imedhamiria kutetea mataji yake yote ya ndani
Ngao ya Jamii tayari iko mikononi, dalili njema zinaonekana kwenye ligi kuu, Yanga ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama nane huku zikiwa zimesalia mechi sita kuhitimisha msimu
Kimahesabu Yanga inahitaji kushinda mechi tatu zinazofuata ili kutetea ubingwa. Kama Wananchi watashinda mehci dhidi ya Kagera Sugar, Simba na Singida Big Stars basi hesabu zitakamilika mapema tu
Lakini iwapo itatokea watani zao Simba watashindwa kupata ushindi katika mechi zao zinazofuata kazi itakuwa rahisi zaidi
Kwenye kombe la FA Wananchi wako hatua ya robo fainali wakitarajiwa kuchuana na Geita Gold
Kama hesabu zitakwenda sawa, Yanga inaweza kufunga msimu ikiwa na mataji manne na kufanya msimu huu kuingia katika kumbukumbu ya klabu
Post a Comment