Yacouba, Mecky Maxime wabeba tuzo NBC

Yacouba, Mecky Maxime wabeba tuzo NBC

Yacouba, Mecky Maxime wabeba tuzo NBC

Yacouba, Mecky Maxime wabeba tuzo NBC

Yacouba, Mecky Maxime wabeba tuzo NBC

Mshambuliaji wa klabu ya Ihefu SC, Yacouba Sogne amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi February wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2022/2023, huku Mecky Maxime wa Kagera Sugar akichaguliwa Kocha Bora wa mwezi huo.

Yacouba amechukua tuzo hiyo baada ya kuwashinda Medie Kagere wa Singida Big Stars na Elias Maguli wa Geita Gold alioingia nao Fainali katika mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).

Kwa mwezi Februari, Yacouba alionesha kiwango kizuri ikiwa ni pamoja na kufunga mabao mawili na kuhusika katika upatikanaji wa bao moja kwenye michezo miwili aliyocheza.

Ihefu kwa mwezi huo ilicheza michezo mitatu ikishinda miwili na kutoka sare mmoja na kupanda kutoka nafasi ya 11 hadi ya 8.Yacouba Mecky Maxime wabeba tuzo NBC

Kwa upande wa Maxime yeye aliwashinda Nasreddine Nabi wa Young Africans na Fikirini Elias wa Coastal Union, ambapo kwa mwezi February, Kagera Sugar ilicheza michezo mitatu na kushinda miwili dhidi ya Namungo bao 1-0 na Ruvu Shooting bao 0-1, ikatoka suluhu na Polisi Tanzania hivyo kujikusanyia alama saba na kupanda kutoka nafasi ya saba hadi ya sita katika Msimamo wa Ligi hiyo yenye timu 16.

Pia Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Highland Estates uliopo Mbarali mkoani Mbeya, Omari Malule kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi February, kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

The post Yacouba, Mecky Maxime wabeba tuzo NBC appeared first on Nijuze Mpya.



from Michezo – Nijuze Mpya https://ift.tt/j208Zr6
via IFTTT

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post