Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mlinzi wa kushoto wa Yanga Joyce Lomalisa ameendelea kuwaborakutokana na kiwango bora anachoonyesha katika kikosi cha Yanga
Kwa sasa unaweza kusema Lomalisa ndiye mchezaji mahiri zaidi upande wa kushoto katika ligi kuu ya NBC
Lomalisa ametajwa kwenye kikosi cha wiki cha CAF kwa michuano ya kombe la Shirikisho sambamba na mshambuliaji Kennedy Musonda
Mcongomani huyo pia alijumuishwa kwenye kikosi cha CAF cha Shirikisho baada ya mechi za raundi ya nne
Utofauti wa Lomalisa na walinzi wengi wa pembeni ni uwezo wake mkubwa wa kupanda na kushuka
Ukiangalia mchezo uliopita dhidi ya US Monastir, Lomalisa ni kama alikuwa akicheza winga akimpa uhuru Kennedy Musonda kuingia ndani kuungana na Fiston Mayele pale timu inaposhambulia
Lomalisa ndiye mchezaji aliyepiga krosi nyingi zaidi katika mchezo huo (7), takwimu zikimuonyesha kuwa mchezaji aliyehusika katika mashambulizi mengi ya Yanga
Wakati mwingine Nabi anaweza kumtumia kama winga na huenda akawa na madhara zaidi akitumika katika nafasi hiyo kutokana na aina yake ya uchezaji
Post a Comment