Wachezaji 10 bora wa soka wa wakati wote 2023 |
Makala hii ina taarifa zote juu ya Wachezaji 10 bora wa soka wa wakati wote 2023,wachezaji bora duniani 2023,mchezaji bora kombe la dunia 2023,tuzo ya mchezaji bora wa dunia.
Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Wachezaji 10 bora wa soka wa wakati wote 2023
Katika makala haya, tumejaribu kufanya hivyo. Ingawa imekuwa si kazi rahisi, tumejaribu kugawanya uteuzi katika vipengele vitatu: Uwezo wa kushinda mechi, uchezaji wa muda mrefu, na kucheza chini ya presha, twende sasa.
#10. Michel Platini
Namba 10 kwenye orodha hii ni Michel Platini. Ufaransa wanaweza kumchukulia mchezaji wao bora kuwahi kutokea ni Zinedine Zidane, lakini kabla ya gwiji huyo wa Real Madrid kufanya uchawi wake, 'Les Bleus' hao walikuwa na mchezaji mwingine mwenye kipaji zaidi ambaye ni Platini.
Akiwa amepewa sifa ya kuifanya Ufaransa kuwa nchi yenye nguvu duniani katika soka, mchezaji huyo alifurahia maisha marefu na yenye manufaa kwa klabu na nchi. Akicheza namba 10, Platini mara zote alionyesha ubora wa hali ya juu kwa kufunga mabao kadhaa muhimu katika maisha yake yote.
Mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or kwa miaka mitatu mfululizo (1983, 84, 85), Mfaransa huyo alifikia kilele cha mchezo wake alipoiongoza Ufaransa kutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 1984 (Euro).
Baada ya kuiongoza Ufaransa kutwaa taji lao la kwanza kubwa la kimataifa na kushinda mataji ya ligi akiwa na Juventus na St Etienne, Platini alistaafu alipokuwa bado kwenye kilele cha kucheza mwaka 1987.
#9. Johan Cruyff
Hakuna mchezaji na mtu katika historia ya mchezo huu aliyotoa mchango mkubwa zaidi kama Johan Cruyff. Ndiye mwanzilishi wa staili maarufu ya mchezo wa soka ya 'tatal football’ kwa Ajax, Barcelona na timu ya Taifa ya Uholanzi.
Mshindi wa Ballon d'Or mara tatu katika maisha yake (1971, 73 na 74), Cruyff aliunda urithi wake kwa mara ya kwanza akiwa Ajax, ambapo aliwaongoza wababe hao wa Uholanzi kutwaa mataji mengi ya ligi na matatu ya Ulaya.
Zaidi ni kwamba, Cruyff anakumbukwa zaidi katika zama za kisasa kwa mabadiliko aliyoleta Barcelona.
Akiwaongoza wababe hao wa Katalunya kutwaa taji lao la kwanza la ligi baada ya miaka 14 mara tu baada ya kujiunga nao. Cruyff anachukuliwa kuwa shujaa na ndiye aliyeanzisha kwa mara ya kwanza staili ya tiki-taka na soka maridadi pale kwenye Uwanja wa Camp Nou.
Cruyff pia alikuwa sehemu ya timu bora zaidi kuwahi kushindwa kutwaa Kombe la Dunia, wakati timu hiyo ya Uholanzi ilipomaliza nafasi ya pili huku Ujerumani Magharibi ikilibeba taji hilo mwaka 1974.
Mwaka 1984 aliiongoza Feyenoord kutwaa taji la ligi, na alikuwa hadithi ya kweli ya mchezo ambaye alikaa katika kiwango cha juu sana kwa miaka 20.
#8. Ronaldo Nazario
Mchezaji anapoichezea Barcelona, Real Madrid, Inter Milan na AC Milan na bado akiwa hachukiwi, unajua ni kitu cha kipekee. Ronaldo Nazario, ambaye pia anajulikana kama 'Fenomeno' huenda ndiye mshambuliaji wa kiwango cha juu zaidi kuwahi kucheza mchezo huo.
Tangu Ronaldo alipoingia uwanjani kama kijana akiwa na umri wa miaka 17, huko Cruzeiro, hakukuwa na shaka kwamba mshambuliaji huyo wa Brazil alikusudiwa kupata mambo makubwa kwenye mchezo huo. Baada ya kucheza soka la Ulaya akiwa na PSV, Ronaldo huenda alikuwa na msimu wa kipekee zaidi wa maisha yake kule Barcelona, ambapo aliimarisha urithi wake kama moja ya vipaji vikubwa zaidi ambavyo mchezo huwa umewahi kushuhudia.
Mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or mwaka 1997 na 2002, mshambuliaji huyo wa Brazil, labda anakumbukwa zaidi kwa uchezaji wake katika Kombe la Dunia la 1998 na 2002 akiwa na timu ya Taifa ya Brazil.
Mwaka 1998, Ronaldo alikuwa mmoja wa wachezaji bora katika mashindano hayo, akifunga mabao manne kusaidia matatu. Hata hivyo, baada ya kupata degedege saa chache kabla ya mchezo wa fainali, hakuwa katika kiwango bora wakati Brazil ilipofungwa na Ufaransa kwenye fainali.
Mwaka 2002 hadithi ilikuwa tofauti. Akirejea kutoka kwenye jeraha, Ronaldo aliiibuka kuwa mfungaji bora kwenye michuano ya Kombe la Dunia kule Japan na Korea Kusini, akifunga mabao nane na kushinda Kiatu cha Dhahabu.
#7. Alfredo Di Stefano
Mchezaji bora kabisa wa Real Madrid na sehemu muhimu ya utawala wao katika miaka ya 1950, Alfredo Di Stefano alikuwa na maisha marefu ya miaka 20 ambapo alikuwa miongoni mwa wanasoka bora duniani kwa muda wote.
Di Stefano anayejulikana sana kwa mafanikio yake akiwa na Real Madrid, alifunga mabao 307 katika mechi 396 na kushinda mataji 15 makubwa akiwa na 'Los Blancos' hao, yakiwamo matano mfululizo ya Ulaya.
Akicheza kama mshambuliaji msaidizi au kiungo mkabaji pamoja na Puskas na Gento, Di Stefano alikuwa kwenye kiwango bora kila wakati kwenye mechi kubwa na anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji pekee kufunga katika fainali tano za Kombe la Ulaya.
Uchezaji bora wa gwiji huyo wa Real Madrid huenda ulikuja katika ushindi wa 7-3 wa fainali dhidi ya Eintracht Frankfurt, ambapo alitawala mchezo na kudhibiti kila kitu uwanjani.
Watu wengi bado wanamchukulia Di Stefano kuwa mchezaji bora wa
Argentina kuwahi kutokea, bora zaidi ya Diego Maradona na Lionel Messi.
Mchezaji kamili ambaye angeweza kucheza katika nafasi nyingi kwa
urahisi.
Kwa bahati mbaya hakuwahi kupata nafasi ya kucheza Kombe la Dunia.
#6. Garrincha
Mshindi wa Kombe la Dunia mara mbili na kuchukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji wenye vipaji zaidi kuwahi kutokea, Garrincha alikuwa namba saba kwa Brazil na klabu yake ya Botafogo. Kuanzia mwaka 1953-1965, Garrincha alitumbuiza umma wa Brazili kwa ustadi wake na mbwembwe, mara nyingi akiwaletea watu furaha tele kwa njia ya kipekee aliyocheza soka.
Garrincha alicheza mechi yake ya kwanza ya Kombe la Dunia akiwa na Brazil mwaka 1958 na mara moja akajitambulisha kama mmoja wa wachezaji bora zaidi ulimwenguni, akifunga na kusaidia mabao mengi kwa wachezaji wenzake kama Vava na Pele.
Katika Kombe la Dunia la mwaka 1962, Garrincha aliiongoza Brazil kutokana na kukosekana kwa Pele na alitajwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo.
Wakati mzuri zaidi wa Mbrazil huyo labda ulikuwa katika nusu fainali ya 1962 dhidi ya Chile, wakati alifunga mabao mawili ya kushangaza.
Kwa bahati mbaya, ulevi na majeraha ya Garrincha yalikatisha kipaji chake. Bado, watu wa Brazil watamkumbuka kila wakati gwiji huyo wa miguu yenye matege ya kupinda na uwezo wake wa kufurahisha siku yao kwa jinsi alivyocheza mchezo huo mzuri.
Tazama pia timu zilizotinga robo fainali ASFC HAPA
#5. Zinedine Zidane
Mshindi wa Ballon d'Or mwaka wa 1998, Zidane alikuwa na kazi yenye mafanikio makubwa Juventus na Real Madrid. Hata hivyo, Zidane alikuja kutambulika kwa mara ya kwanza kama mchezaji wa hali ya juu duniani kutokana na uchezaji wake dhidi ya Brazil katika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1998.
Akifunga mabao mawili kwa kichwa katika fainali, Zidane aliipa Ufaransa ushindi wao wa kwanza wa Kombe la Dunia, hivyo kumfanya kuwa shujaa na nyota wa usiku mmoja.
Alifuatia kwa uchezaji mzuri katika Euro 2000, ambapo Ufaransa iliishinda Italia na kutawazwa kuwa mchezaji bora wa mashindano.
Baada ya kubadili rekodi ya dunia wakati huo kwenda Real Madrid, Zidane hivi karibuni alionyesha kiwango chake na kuwa mmoja wa wachezaji bora wa safu iliyojaa nyota. Wakati wake maarufu akiwa amevalia jezi nyeupe ulikuja katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2001-02 dhidi ya Bayer Leverkusen.
Huku matokeo yakiwa 0-0, Zidane alionyesha mbinu ya ajabu ya kukwamisha shuti kali la mguu wa kushoto kutoka nje ya eneo la hatari akiwa hajaliangalia goli. Moja ya mabao mazuri katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mfaransa huyo alionyesha kwamba anaweza kutegemewa kila wakati katika hatua muhimu.
Hadi alipostaafu mchezo huo mwaka 2006, Zidane alibakia kuwa miongoni mwa wachezaji bora zaidi duniani. Ukiacha rafu ya kumpiga kichwa mchezaji kwenye fainali ya Kombe la Dunia ya 2006, Mfaransa huyo mashuhuri alikuwa mchezaji aliyefurahi sana akiwa kwenye hatua ya mashindano makubwa.
Kwa maisha yake marefu ya ajabu na uchezaji wake wa ajabu katika fainali ya Kombe la Dunia la 1998, mashindano ya Ulaya 2000 na fainali ya Ligi ya Mabingwa 2002, Zidane anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa wakati wote.
#4. Cristiano Ronaldo
Mtoto mwenye kipaji cha hali ya juu katika klabu ya Sporting CP, Cristiano Ronaldo aligunduliwa na Sir Alex Ferguson na ni huko Manchester United, ambapo nyota huyo wa Ureno aliimarisha urithi wake kama mmoja wa wachezaji wakubwa wa kizazi hiki.
Azma kali ya kuwa bora, Ronaldo, pamoja na ujasiri na dhamira yake pamoja na kipaji chake cha hali ya juu, imekuwa moja ya majina yanayotambulika katika soka la ulimwengu wa leo.
Ingawa alijipatia umaarufu kama nyota wa Manchester United, ilikuwa ni Real Madrid ambapo aliimarisha hadhi yake ya kuwa mchezaji bora wa muda wote.
Iwe ni kufunga penalti ya mwisho katika mikwaju ya penalti ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa au kufunga bao muhimu katika nusu fainali ya Euro 2016, Ronaldo amekuwa akiuonyesha ulimwengu kile anachoweza.
Pamoja na mchezo wake kwa takriban miaka 16 sasa, mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d'Or mara tano, aliendelea kuifungia Juventus mabao baada ya kuondoka Madrid na kwenda Turin msimu wa majira ya joto wa 2018.
Kwa sasa, amerejea Manchester majira ya joto yaliyopita. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37, hivi majuzi alikuwa mfungaji bora zaidi katika soka la kulipwa (mabao 807) na hat-trick yake dhidi ya Tottenham.
#3. Lionel Messi
Lionel Messi pamoja na Cristiano Ronaldo, bila shaka ni miongoni mwa wachezaji wakubwa zaidi wa kizazi hiki. Akiwa ameonekana kama mtoto mpya wa La Masia mwaka wa 2005, Messi, kwanza chini ya ulezi wa Frank Rijkaard na kisha, muhimu zaidi, chini ya Pep Guardiola, alijidhihirisha kuwa mmoja wa wachezaji wakubwa waliowahi kupamba mchezo huo.
Wakati Messi amefunga katika kila aina ya mechi muhimu za klabu - fainali za Ligi ya Mabingwa, nusu fainali, Fainali za Copa del Rey (Kombe la Mfalme), Clasicos dhidi ya Real Madrid, alikuwa na shida wakati akiichezea Argentina.
Baada ya kupoteza fainali tatu mfululizo akiwa na timu ya taifa, Messi alistaafu kuichezea timu ya taifa kwa muda mfupi, kisha akarejea miezi miwili baadaye na hatimaye alimaliza ukame wake na Argentina kwa kunyanyua Copa America mwaka 2021.
Haijalishi atafanya nini kuanzia sasa, Messi atazingatiwa kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi wa wakati wote. Mchezaji pekee aliyeshinda Ballon d'Or mara saba, mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, aliondoka Barcelona majira ya kiangazi mwaka jana katika uhamisho wa kushtukiza na kujiunga na PSG.
#2. Diego Maradona
Diego Maradona kama mchezaji na mtu anayekumbukwa zaidi katika mechi dhidi ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia la 1986. Nyota huyo wa Argentina, aliichachafya safu ya ulinzi ya Uingereza na kufunga mabao makubwa zaidi ya wakati wote.
Akiwa na kipaji cha hali ya juu, Maradona angeweza kufanya mambo na mpira wa miguu ambao wanadamu hawakuweza hata kuota. El Diego alikuwa nyota wa ushindi maarufu wa Argentina wa Kombe la Dunia mwaka 1986.
Maradona pia alifanya yake kwenye kazi ya Klabu Ulaya, kwanza Barcelona na kisha Napoli. Ingawa mchezaji huyo mashuhuri alishinda tu Copa del Rey na Supercopa Espana wakati alipokuwa Barcelona.
Akiwa Napoli, Maradona alishinda mataji mawili ya Serie A. Hadi leo Maradona bado ni mwana kipenzi wa Napoli na anachukuliwa kuwa mchezaji bora zaidi kuwahi kucheza Ulaya. Maradona aliaga dunia mwaka 2020 kutokana na mshtuko wa moyo.
#1. Pele
Gwiji wa Brazil, Pele anachukuliwa kuwa mwanasoka bora zaidi wa wakati wote. Hakuna mchezaji aliyeshinda Kombe la Dunia zaidi yake, na hiyo pekee inapaswa kutosha kuhalalisha kujumuishwa kwa Mbrazil huyo katika kilele cha orodha hii.
Mfungaji bora zaidi, Pele pia alikuwa kitovu cha ushambuliaji kwa klabu na nchi. Takwimu zake za mabao ni za kushangaza; ndiye mchezaji pekee aliyefunga zaidi ya mabao 1200.
Mchezaji mdogo zaidi kuwahi kutokea (miaka 17 na siku 249) kufunga katika Kombe la Dunia. Pele alifunga mara mbili katika fainali ya Kombe la Dunia 1958 dhidi ya Uswisi.
wachezaji bora duniani 2023 | mchezaji bora kombe la dunia 2023
Ingawa aliweza kucheza mechi moja pekee katika Kombe la Dunia la mwaka 1962 kwa sababu ya jeraha, ilikuwa mwaka 1970 ambapo aliimarisha urithi wake kama mchezaji bora zaidi wa wakati wote. Wakicheza kandanda maridadi, Brazil ilitawala mashindano hayo, huku Pele akishinda tuzo ya Mpira wa Dhahabu na Mchezaji Bora.
Post a Comment