Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Jumapili Yanga itashuka dimba la Mazembe kuwakabili wenyeji wao TP Mazembe katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Yanga tayari imewasili Lubumbashi usiku wa kuamkia leo kuelekea mtanange huo wa kukata na shoka
Hii ni mechi muhimu kwa Yanga kusaka ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kumaliza kinara wa kundi D
Za chini ya kapeti ni kuwa kuna biashara itafanyika huko DR Congo baada ya mechi hiyo
Miongoni mwa watu waliosafiri katika msafara wa Yanga ni pamoja na Ghalib Said Mohammed 'GSM' ambaye huwa ni nadra sasa kuambatana na kikosi cha Yanga
Kupitia ujumbe uliowekwa na Yanga kwenye kurasa zao rasmi kwenye mitandao ya kijamii, walibainisha kuwa GSM amesafiri na timu DR Congo je Wananchi wanadhani watarudi na nani?
Yanga inahusishwa kumuwania winga hatari wa TP Mazembe Felipe Kinzumbi ambaye msimu huu amekuwa mchezaji bora zaidi katika kikosi cha Mazembe
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said kama ilivyo kawaida yake, alianza harakati za kumnasa Kinzumbi baada ya mchezo ambao TP Mazembe walikubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Yanga uwanja wa Benjamin Mkapa
Wakati Yanga ikiendelea na harakati za kuitafuta nusu fainali ya kombe la Shirikisho, mabosi wanaendelea kusuka kikosi kwa ajili ya kufanya makubwa zaidi msimu ujao
Post a Comment