Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Huu ni mchezo muhimu kwa Yanga kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kumaliza katika nafasi ya kwanza kundi D
Yanga na US Monastir zinachuana kuwania nafasi hiyo Wananchi wakiwa kileleni kwa faida ya mabao timu zote zikiwa na alama 10
Baada ya ushindi wa mabao 3-1 ambao Yanga waliupata dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, ni wazi TP Mazembe nao hawatakuwa wanyonge katika uwanja wao wa nyumbani licha ya kuwa matokeo yoyote watakayopata hayatakuwa na faida kwao
Yanga kuwa na idadi kubwa ya wachezaji wenye asili ya DR Congo, imeongeza ushindani kwani mechi hii itakuwa ni dabi ndani ya DR Congo
Kwa sasa Yanga ni timu maarufu sana DR Congo, mashabiki wa AS Vita ambao ni timu pinzani ya TP Mazembe, wanatarajia kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili kuishangilia Yanga
Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema wanatarajia kuzindua Tawi la Yanga katika Mji wa Lubumbashi wakiwa tayari wamesajili Wanachama zaidi ya 100 ambao wakatabidhiwa kadi zao
Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele amesema mashabiki wa soka DR Congo wameisubiri kwa shauku kubwa Yanga akiamini watapata sapoti kubwa
"Kwa sisi wachezaji ambao ni Wacongo hii ni kama dabi. Hii itakuwa dabi ya pili baada ya ile tuliyocheza Dar es salaam ambao tuliwafunga 3-1. Mashabiki wamesubiri mchezo huu na watakuja kutushangilia," alisema Mayele ambaye ataungana na wenzake huko DR Congo
Yanga pia imesafiri na mashabiki wake kutoka jijini Dar es salaam ambao wanatarajiwa kuwasili leo ili kuongeza hamasa katika mchezo huo utakaopigwa Jumapili April 02 saa 10 jioni
Nyota wa Yanga waliowahi kuitumikia AS Vita ambao kwa kiasi kikubwa wameshawishi mashabiki wengi hasa wa AS Vita kuwaunga mkoni ni Mayele, Djuma Shaban, Joyce Lomalisa, Yannick Bangala, Tuisila Kisinda na Jesus Moloko
Post a Comment