Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice, 24, ndiye mchezaji anayesakwa zaidi na Arsenal msimu huu wa joto na kuna imani inayoongezeka kuwa wanaweza kufanikiwa kiwashinda Chelsea, Manchester City na Manchester United ili kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza. (Evening Standard)
Real Madrid wamemfanya kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham, 19, kuwa usajili wao wa kipaumbele, hata hivyo miamba hao wa Hispania pia wanavutiwa na mlinzi wa Chelsea mwenye umri wa miaka 23 Reece James. (AS)
Manchester United inawafuatilia mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt ya Ufaransa Randal Kolo Muani, 24, na mshambuliaji wa Atalanta wa Denmark Rasmus Hojlund, 20 iwapo wataaambiwa bei kubwa kwa mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 29 chaguo lao la kwanza. (Manchester Evening News)
United huenda ikakosa kumsajili kiungo wa Austria Marcel Sabitzer kwa usajili wa kudumu baada ya mkataba wake wa mkopo kumalizika huku meneja mpya wa Bayern Munich Thomas Tuchel akiamua kumbakisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Sun)
Mjerumani Julian Nagelsmann, 35, na Muargentina Mauricio Pochettino, 51, wako tayari kurithi mikoba ya Muitaliano Antonio Conte katika klabu ya Tottenham - hata hivyo mameneja wote wawili watasubiri kuona kama kibarua cha Real Madrid kitapatikana katika msimu wa joto. (90min)
Kocha wa zamani wa Hispania Luis Enrique, 52, anasema angependa kufundisha ligi kuu England akiwa na timu ambayo inaweza kufanya mambo makubwa. (Cadena SER)
Kiungo wa kati wa Ujerumani Ilkay Gundogan, 32, yuko tayari kuondoka Manchester City na kujiunga na Barcelona kwa uhamisho wa bure mwishoni mwa msimu huu. (Football Insider)
Barcelona wataendeleza mpango wa kumnunua Gundogan baada ya kufikia makubaliano ya mdomo kumsaini beki wa kati wa Athletic Bilbao raia wa Hispania Inigo Martinez, 31. (ESPN).
Barcelona itakabiliana na ushindani kutoka kwa Arsenal na Chelsea katika mbio za kumnunua mshambuliaji wa Athletico Paranaense wa Brazil Vitor Roque, 18. (Sport)
Manchester City na Paris St-Germain wamewasilisha ombi la kwanza kwa mlinzi wa Hajduk Split mwenye umri wa miaka 16 kutoka Croatia Luka Vuskovic. (90min)
Kipa wa Hispania David de Gea, 32, amekataa ofa ya kwanza ya Manchester United ya kandarasi mpya. (Athletic)
Mshambulizi wa kimataifa wa England Marcus Rashford, 25, amekanusha ripoti kwamba anataka mkataba mpya, wenye thamani ya £500,000 kwa wiki ili kusalia Manchester United, akisema habari hizo ni kama upuuzi mtupu (Athletic)
BBC
Post a Comment