Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Manchester United wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 80 kumnunua mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 29, baada ya mtendaji mkuu wa klabu Richard Arnold kuidhinisha mpango huo. (Star)
Bayern Munich wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea na England Mason Mount, 24. (Times)
Manchester United hawajachukua hatua zozote zaidi katika kuafiki mkataba mpya kwa mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 25. (Athletic )
Manchester City bado wanamngoja kiungo wa kati wa Ujerumani Ilkay Gundogan kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake, huku Barcelona wakitamani kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kwa uhamisho wa bure. (Fabrizio Romano)
Iwapo Gundogan ataondoka, City inamfikiria kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham, 19, na kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Florian Wirtz, 19, kama wachezaji wanaoweza kuchukua nafasi yake. (Football Insider)
Vilabu vinavyovutiwa na Roberto de Zerbi vitalazimika kulipa kiasi fulani kwa Brighton kwa ajili ya meneja huyo wa Italia, na makubaliano yanaweza tu kufanywa katika majira ya joto, si wakati wa huu msimu ukiendelea. (Fabrizio Romano) Wakati huo huo, De Zerbi anataka udhibiti zaidi na fedha zaidi katika mipango ya uhamisho ya Seagulls. (Mail)
Chelsea bado hawajaanza mazungumzo ya mkataba mpya na kiungo wa kati wa Croatia Mateo Kovacic, huku Manchester City wakimtaka. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amebakiza miezi 16 katika mkataba wake wa sasa. (Standard)
Liverpool wako tayari kulipa zaidi ya £60m kumnunua beki wa kati wa Napoli na Korea Kusini Kim Min-jae, 26, ambaye pia anasakwa na Manchester United. (Rai, via Four Four Two)
Arsenal wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Denmark Jesper Lindstrom, 23, ambaye Eintracht Frankfurt itamruhusu kuondoka kwa ada ya takriban euro 30m. (Sport 1)
Chelsea wanatazamiwa kumuweka sokoni kiungo Muingereza Ruben Loftus-Cheek, 27, mwishoni mwa msimu huu. (Football Insider)
Vilabu kadhaa vya Ligi kuu ya England, vikiwemo Leicester, Fulham na Wolves, vinamfuatilia kiungo wa kati wa Lorient na Ufaransa walio chini ya umri wa miaka 21 Enzo le Fee baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kuthibitisha kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo ya Ufaransa msimu huu. (90Min)
Tottenham wamefikia makubaliano ya awali ya mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Herbie James, 16, kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka akademi ya Manchester City. (Football London)
BBC
Post a Comment