Manchester United wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Benfica na Ureno Goncalo Ramos, 21, ambaye ana kipengele cha kuondoka cha euro milioni 120 (£105.6m). (Record, via Goal)
Mshambulizi Evan Ferguson, 18, atakataa kuhamia Manchester United kwa sababu mchezaji huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland anadhani kusalia Brighton kutakuwa bora zaidi kwa maendeleo yake. (Sun)
Wakati huo huo, Manchester United watamfikiria kipa wa Brentford Mhispania David Raya, 27, kama mbadala wa mtani wake David de Gea, 32, ambaye bado hajakubali kusaini mkataba mpya. (Give Me Sport)
Chelsea wako tayari kutoa euro milioni 100 kumnunua mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 24, wa Napoli. (Football Insider)
Chelsea wako kwenye mazungumzo na kiungo wa kati wa Ufaransa N'Golo Kante, 31, kuhusu kandarasi mpya ya miaka miwili, kukiwa na chaguo la mwaka zaidi Stamford Bridge. (Fabrizio Romano)
The Blues wamesikitishwa na meneja wa zamani, Mjerumani Thomas Tuchel, kwa kuweka hadharani nia yake ya kumchukua kocha wa kiwango cha juu wa Uingereza Anthony Barry kwenda Bayern Munich. (Telegraph)
Arsenal wataipatia kipaumbele jaribio lingine la kumsajili kiungo wa kati wa Brighton na Ecuador Moises Caicedo, 21, msimu wa joto. (Football transfers)
Aston Villa, Newcastle na Brighton wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Alex Oxlade-Chamberlain, 29, ambaye mkataba wake na Liverpool unamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Mail)
Barcelona wamejiondoa katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Ureno na Wolves Ruben Neves, 26, msimu huu. (Fichajes - kwa Kihispania)
Kiungo wa kati wa Uhispania Sergio Busquets, 34, bado hajakubali mkataba mpya na Barcelona na anaweza kuhamia Ligi Kuu ya Soka. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
Chelsea na Arsenal watamenyana katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Everton na Ubelgiji Amadou Onana, 21, baada ya kuanza vyema soka lake Goodison Park. (Fichajes - kwa Kihispania)
BBC
Post a Comment