Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mshambuliaji wa Fulham na timu ya taifa ya Serbia Aleksandar Mitrovic, 28, alikuwa akisakwa na Manchester United kabla ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu Old Trafford kwa kumsukuma mwamuzi Chris Kavanagh. (Daily Star)
Manchester United pia wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brighton na Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 18. (Football Insider)
United "wana nia ya dhati" ya kumsajili mshambuliaji wa Denmark Rasmus Hojlund, 20, ambaye anachezea Atalanta. (Ekstra Bladet, via Spoti Shahidi) Manchester City wako tayari kumpa mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 22, kandarasi mpya yenye thamani ya pauni 500,000 kwa wiki ili kuzuia nia ya Real Madrid wanaomnyatia. (Sun)
Leeds United wana nia ya kumsajili tena kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 27, msimu huu wa joto licha ya kwamba alijiunga na Manchester City pekee mwaka jana. (Daily Star)
Brighton hawatamruhusu meneja wao Roberto de Zerbi, 43, kuondoka kujiunga na Tottenham Hotspur wanaomtaka achukue mikoba ya bosi wao wa sasa, Muitaliano mwenzake Antonio Conte mwenye umri wa miaka 53. (Press)
Hakuna mazungumzo yaliyokuwa yamefanyika kati ya Tottenham na Mjerumani Thomas Tuchel, 49, kabla ya kocha huyo wa zamani wa Chelsea kuteuliwa kuwa meneja wa Bayern Munich siku ya Ijumaa. (Evening Standard)
Kiungo wa kati wa England James Ward-Prowse, 28, bila shaka ataondoka Southampton msimu huu wa joto ikiwa Saints watashuka daraja, huku Tottenham wakitaka kumsajili. (Football Insider)
Arsenal ni miongoni mwa klabu zinazohitaji kumnunua kiungo wa kati wa Southampton raia wa Ubelgiji Romeo Lavia, 19. (Fabrizio Romano)
Inter Milan wanafuatilia sana hali ya Pierre-Emerick Aubameyang katika klabu ya Chelsea na wanaweza kumnunua mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Gabon. (Gazzetta dello Sport)
Kiungo Luka Modric, 37, amepuuza tetesi za kuhamia klabu ya Saudi Arabia huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia akisema anataka kustaafia Real Madrid. (Mail)
Tottenham wanavutiwa na kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Manuel Ugarte, 21. (Mirror) Leeds pia wametuma maskauti kumtazama mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay. (O Jogo via Goal)
West Ham wanamtaka mshambuliaji wa Coventry na Sweden Viktor Gyokeres, 24, ambaye thamani yake ni karibu £20m. (Sun) Brentford, Crystal Palace, Everton, Leeds na Leicester zote pia zinamfuatilia Gyokeres. (90Min)
BBC
Post a Comment