Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Manchester United wako tayari kumuuza nahodha na beki wa kati wa England Harry Maguire, 30, na mlinzi wa Uswisi Victor Lindelof, 28, msimu huu. (Football Insider)
Meneja Jurgen Klopp anataka Liverpool kumpa kiungo mkongwe wa Uingereza James Milner, 37, mkataba mpya. (Football Insider)
Chelsea wana nia ya kumnunua kipa wa Inter Milan na Cameroon Andre Onana, 26, msimu wa joto. (InterLive, via Fichajes - in Spanish)
Arsenal wanataka kumsajili beki wa kulia wa Galatasaray Mfaransa Sacha Boey, 22. (Aksam - in Turkish)
Kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Marco Reus, 33, anataka kusalia Borussia Dortmund, ambako ni nahodha, hadi mwisho taaluma yake . (Sky Germany - in German)
Chelsea na Newcastle wote wanamfuatilia mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Brahim Diaz. Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa sasa yuko kwa mkopo huko AC Milan kutoka Real Madrid lakini anaweza kupatikana mwishoni mwa msimu huu. (Sun)
Tottenham wanaweza kufufua nia yao ya kumnunua beki wa kati wa Napoli na Korea Kusini Kim Min-jae, 26, msimu huu. (Football Insider)
Everton watamnunua mshambuliaji wa West Ham kutoka Jamaica Michail Antonio, 32, msimu wa joto, iwapo wataepuka kushushwa daraja. (Sun)
Kiungo wa kati wa Ghana Mohammed Kudus, 22, anatumai kusalia Ajax hadi mwisho wa msimu huu licha ya Manchester United, Arsenal na Liverpool kumtaka. (De Telegraaf, via 90min)
Besiktas wanajiandaa kuanzisha kipengee cha kununu kununua katika mkataba wao wa mkopo wa beki wa West Ham kutoka Congo Arthur Masuaku, 29. (Fanatik, via Inside Futbol)
Kocha wa zamani wa Everton Frank Lampard yuko tayari kwa nafasi yake nyingine ya ukocha, karibu miezi miwili tangu atimuliwe na The Toffees. (Sun)
BBC
Post a Comment