Real Madrid wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Manchester City na Norway Erling Haaland, 22, msimu wa joto kama sehemu ya mpango wa kuleta kizazi kipya cha nyota wachanga ambao pia ni pamoja na kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Uingereza Jude Bellingham, 19. (Independent).
Beki wa Manchester United na Muingereza Harry Maguire, 30, analengwa kwa pauni milioni 50 na Paris St-Germain msimu wa joto. (Sun)
Rais wa heshima wa Bayern Munich Uli Hoeness anasema "itakuwa jambo la kustaajabisha" ikiwa mabingwa hao wa Ujerumani watamnunua mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 29, na kwamba siku ambayo klabu hiyo itatumia euro 100m katika uhamisho "inakuja". (Sky Sport Germany - In Germany)
Feisal, Yanga na GSM kukaa meza Moja kuyamaliza ishu Iko hivi bofya hapa kusoma
Manchester United wamemuongeza kiungo wa kati wa Chelsea na Uingereza Mason Mount, 24, kwenye orodha ya wachezaji wanaotarajiwa kusajiliwa msimu wa joto. {Guardian)
Mauricio Pochettino ameiambia Tottenham kwamba ana nia ya kurejea na kuchukua nafasi ya Antonio Conte kama meneja, lakini Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 51 pia ana chaguo kutoka kwa vilabu nje ya England. (talkSPORT)
Tottenham itajadili sifa za Pochettino na Thomas Tuchel kama wasimamizi wanaoweza kurithi nafasi ya Conte, ambaye klabu hiyo imepanga kuachana naye. (Guradian)
Kocha wa Brentford, Thomas Frank na Marco Silva wa Fulham pia wako kwenye orodha ya wachezaji watano walioteuliwa kuchukua nafasi ya Conte huko Tottenham. (Independent)
Manchester City wako tayari kumuuza mlinzi wa Uhispania Aymeric Laporte, 28, msimu huu wa joto ikiwa klabu hiyo inaweza kupata mchezaji wa kiwango cha juu. (Football Insider)
Manchester United ni moja ya klabu zinazovutiwa na mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 29, ambaye anaweza kusajiliwa kwa pauni milioni 11 msimu wa joto licha ya kujiunga na Roma mwaka jana pekee. (Goal)
Manchester United pia wamejiunga na orodha inayovutiwa na mlinda mlango wa Brentford David Raya, huku Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 27 akitarajiwa kuondoka The Bees baada ya kukataa kandarasi mpya. (talkSPORT)
Beki wa pembeni wa Manchester City na Ureno Joao Cancelo, 28, ameibuka kama mchezaji anayelengwa na Barcelona baada ya muda wake wa mkopo Bayern Munich kukamilika msimu wa joto. (Sport – In Hispanic)
Wolves wako tayari kufanya uhamisho mpya wa pauni milioni 20 kumnunua Alex Scott wa Bristol City huku wakipania kuwazidi Tottenham na West Ham katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo huyo Mwingereza mwenye umri wa miaka 19. (Telegraph – Subscription Required)
Mshambulizi wa Argentina Lionel Messi, 35, yuko kwenye mazungumzo ya kusaini mkataba mpya huko Paris St-Germain, lakini mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24, na mshambuliaji wa Brazil Neymar, 31, wanaweza kuondoka kwa mabingwa hao wa Ligue 1 msimu huu. (Mail)
Newcastle United wako tayari kushindana na wapinzani wachache wa Premier League kumsajili kiungo wa kati wa Southampton Muingereza James Ward-Prowse, 28, msimu wa joto. (Football Insider)
Newcastle wako mbioni kuafiki mkataba mpya wa muda mrefu na kiungo wa kati wa Brazil Bruno Guimaraes, 25. (Telegraph - subscription required)
Inter Milan wamempa Edin Dzeko mkataba mpya wa mwaka mmoja lakini mshambuliaji huyo wa Bosnia, 36, anataka mkataba wa miaka miwili ili ajiunge na West Ham, huku fowadi wa Italia Gianluca Scamacca, 24, akijiunga na Inter Milan. (Gazzetta dello Sport – In Itali)
Bayer Leverkusen hawana uwezekano wa kutafuta mkataba wa kudumu kwa winga wa Uingereza Callum Hudson-Odoi, 22, wakati mkopo wake kutoka Chelsea utakapokamilika msimu wa joto. (Sky Sport Germany – In Germany)
Kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25, amejitenga na uwezekano wa kuhamia Manchester United, akisema "ana furahia sana kusalia Barcelona". (RAC1, via Goal)
Leeds wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa Uhispania Ilias Akhomach, 18, mkataba wake utakapokamilika Barcelona msimu huu wa joto. (Sport – In Hispanic)
Arsenal na Chelsea wamejiunga na orodha ya klabu ambazo zimeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Brazil Vitor Roque, 18 kutoka Athletico Paranaense. (90 Min)
Paris St-Germain wanafikiria kumbadilisha mkufunzi Christophe Galtier na kumwingiza kocha wao wa zamani Thomas Tuchel, ambaye bado hana kazi baada ya kutimuliwa na Chelsea Septemba mwaka jana. (Relevo - kwa Kihispania)
BBC
Je unatafuta Ajira tembelea tovuti hii Sasa Kwa matangazo yote ya kazi BOFYA HAPA SASA
Post a Comment