Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imeshindwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Uganda katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2023
Rodgers Mato ndiye aliyewapa Watanzania machungu leo akifunga bao katika dakika ya 90 baada ya Uganda kufanya shambulizi ya kushitukiza
Stars ilihitaji ushindi au hata alama moja ili kujiweka katika nafasi ya kufuzu lakini matokeo hayo yamefanya timu zote ziwe na nafasi
Stars imeendelea kusalia nafasi ya pili ikiwa na alama nne sawa na Uganda timu hizo zikiwa na uwiano sawa wa mabao ya kufunga na kufungwa
Niger inashika nafasi ya mwisho kundi F ikiwa na alama mbili wakati Algeria tayari imefuzu ikiongoza kundi F ikiwa na alama 12
Mchezo utakaofuata kwa Tanzania ni dhidi ya Niger, utapigwa Juni 2023 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Post a Comment