Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Uganda ndio wenyeji wa mchezo huo ambao walilazimika kuupeleka Misri baada ya CAF kukataa viwanja vya Uganda kwa kukosa sifa
Hii ni nafasi ya adimu kwa Tanzania kusaka ushindi katika mchezo ambao ni kama timu zote zitakuwa ugenini
Baada ya Niger kuchapwa mabao 2-1 na Algeria hapo jana, timu itakayoshinda leo itapanda mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi F
Itakuwa mechi ya kwanza kwa kocha Adel Amrouche ambaye alikabidhiwa majukumu ya kuinoa Stars hivi karibuni
Amrouche amesema pamoja na vijana wake kupata muda mfupi wa kufanya mazoezi ya pamoja, wako tayari kwa mchezo huo ambao dhamira yao ni kusaka ushindi
Mchezo wa marudiano utapigwa jijini Dar es salaam siku ya Jumanne, March 28 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Post a Comment