Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Klabu ya Yanga imewatangazia Wanachama na Mashabiki wake fursa ya kusafiri na timu DR Congo kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe ambao utapigwa April 02
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabri mapema leo, Kamwe alisema wanahitaji kwenda kupata ushindi dhidi ya TP Mazembe ili kujihakikishia nafasi ya kwanza kwenye kundi D
"Kama klabu tumeandaa safari, timu itaondoka na Air Tanzania wakati msafara wa mashabiki utaondoka kupitia usafiri wa barabara. Gharama ya safari nzima ni Tsh 700,000/-"
"Muhimu shabiki lazima awe na pasport, masuala mengine yote yatagharamiwa na kiasi hicho cha fedha. Timu itarejea jijini Dar es salaam April 03 baada ya mchezo," alisema Kamwe
Akizungumzia maandalizi ya kikosi, Kamwe amesema wachezaji walipewa mapumziko ya siku tatu na kesho Alhamisi wataripoti Avic Town kuanza maandalizi
Kikosi kitaingia kambini March 27 kujiandaa na mchezo dhidi ya TP Mazembe ambapo safari ya DR Congo itakuwa March 30
Baadhi ya wachezaji wataungana na timu huko DR Congo baada ya kumaliza majukumu yao ya timu za Taifa
Post a Comment