Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Hersi amesema Umoja mshikamano wa viongozi, sapoti ya wanachama na mashabiki umewezesha kufanikisha kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika huku wakiendelea kutimiza malengo ya ndani kwa kushinda Ngao ya Jamii, kuongoza ligi kwa tofauti ya alama nane pia wakitinga robo fainali kombe la Shirikisho la Azam
Hersi amesema wanahitaji Mshikamano na sapoti ya mashabiki kuhakikisha Yanga inashinda mchezo dhidi ya TP Mazembe ili kuongoza kundi D
"Dhamira yetu ilikuwa angalau kutinga hatua ya makundi lakini tumefanikiwa kuvuka na kutinga robo fainali"
"Klabu imeandaa utaratibu wa wanachama na mashabiki kwenda kushiriki mchezo dhidi ya TP Mazembe huko DR COngo ili kuongeza nguvu"
"Hii ni nafasi nzuri kwetu na kihistoria kuongoza kundi gumu katika mashindano ya Shirikisho. Faida kubwa ya kuwa kinara wa kundi ni kuwa; kwenye robo fainali tutapangwa na timu iliyomaliza nafasi ya pili katika kundi jingine na muhimu zaidi tutaanzia ugenini na kisha kumalizia mchezo wa pili nyumbani"
"Tunawaomba Wanachama na mashabiki wetu mchangamkie fursa hii mkawape nguvu wachezaji wetu," alisema Hersi
Jana Yanga ilitangaza nafasi kwa Wananchi kusafiri na kikosi cha Yanga kwenda DR Congo timu ikitarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam March 30. Gharama ya safari kwenda na kurudi ni Tsh 700,000/-
Post a Comment