Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Singida BS jana walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Dodoma Jiji na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika uwanja wa Jamhuri
Za ndani ni kuwa mabosi wa timu hiyo wameanza mipango ya kumng'oa kipa wa Simba Beno Kakolanya
Singida BS wameanza mazungumzo na kipa huyo ambaye mkataba wake unaelekea mwishoni kwa lengo la kumsajili aitumie kuanzia msimu ujao.
Mkataba wa Kakolanya na Simba unaisha mwishoni mwa msimu huu na hadi sasa inadaiwa hakuna makubaliano ya kusaini dili jipya licha ya mabosi wa Msimbazi kuzungumza naye hivi karibuni, hivyo kutoa nafasi kwa kipa huyo namba mbili ndani ya timu hiyo kutafuta changamoto mpya.
Singida BS wamekuwa na changamoto katika eneo lao la magolikipa sasa wakimtegemea Benedict Haule baada ya kumtoa kwa mkopo Metacha Mnata kunako klabu ya Yanga
Post a Comment