Miamba ya Soka la Bongo upande wa Wanawake Simba Queens na Yanga Princesskesho Jumatano (Machi 22) itapapatuana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara Jumatano kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Yanga Princess itakua mwenyeji wa mchezo huo wa Duru la Pili la Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, huku ikijaribu kutafuta Rekodi ya kuwafunga Simba Queens kwa mara nyingine kwenye misimu ya hivi karibuni.
Mchezo wa Duru la Kwanza uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1, Yanga Princess wakitangulia kufunga kupitia kwa Wogu Succes na Simba Queens wakichomoa kwa shuti la Aquino Corozone.
Yanga Princess wanahitaji kushinda mchezo huu kwa kuwa kama watapoteza watakuwa na nafasi ndogo zaidi ya kumaliza Ligi wakiwa mabingwa, kwani watakuwa wamepitwa alama 08 na Simba Queens, huku Fountain Gate Princess na JKT Queens endapo watashinda michezo yao, itakuwa ni utofauti wa alama 07 na 08.
Yanga Princess wamekusanya alama 21 kwenye michezo 11 waliocheza, wakati Simba Queens wamevuna alama 26 kwenye michezo 11 ikilingana na Fountain Gate na JKT Queens zenye alama 25 kila moja.
Yanga Princess wanakwenda kwenye mchezo huu wakiwa na kumbukumbu ya kuvuna alama moja tu kwenye michezo miwili ya waliocheza ugenini. Wakifungwa na Fountain Gate 1-0, kisha kutoka suluhu na Mkwawa Queens.
Post a Comment