Uongozi wa Klabu ya Al Ahly umemueleza CEO wa klabu hiyo kuwa ahakikishe anawaondoa wachezaji watatu katika dirisha lijalo la usajili.
Wachezaji hao ni Luis Miquissone, Bruno Savio na Walter Bwalya ambao wanapaswa kuwa wameondoka.
Kuondoka kwa wachezaji hao ni kutoa fursa kwa klabu kuingiza wachezaji wapya.
Kuachwa kwa Miquissone inaweza kuwa ni habari njema kwa Simba SC ambao mara kadhaa walijaribu kutaka kumrudisha mchezaji huyo lakini inaelezwa malipo makubwa ya mshahara wake yalikuwa kikwazo kwa SImba na hiyo kwenda kwa Mkopo katika klabu ya Abha ya nchini Saudi Arabia.
Miquissone aliuzwa na Simba mwishoni mwa msimu wa mwaka 2020/2021 akiwa ashafanya makubwa na kujitengenezea ufalme wake ndani ya klabu ya Simba.
Post a Comment