Saka mcgezaji Bora wa mwezi march Epl

 

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


Bukayo Saka ametawazwa Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza, akinyakua tuzo hiyo baada ya kuwasaidia viongozi Arsenal kushinda michezo yao yote minne katika kinyang'anyiro hicho mwezi Machi.

Saka alifunga mabao matatu na kuongeza pasi mbili za mabao katika mechi nne alizocheza mwezi huo huku Arsenal wakiandikisha ushindi dhidi ya Everton, Bournemouth, Fulham na Crystal Palace.

Ni Erling Haaland wa Manchester City (33) tu na Harry Kane wa Tottenham (23) ambao wamehusika katika mabao mengi ya Premier League kuliko Saka msimu huu (22).

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, anayechukuliwa kuwa mchezaji bora wa msimu, ndiye mchezaji pekee aliyefikisha idadi ya mabao (12) na asisti (10) katika ligi msimu huu

Akiwa ameisaidia Arsenal kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi nane dhidi ya City huku The Gunners wakiwinda taji lao la kwanza la ligi tangu 2004

Saka alichuana na Alexander Isak, Alexis Mac Allister, Tyrone Mings, Mohamed Salah na mwenzake wa Arsenal Leandro Trossard

Anakuwa nyota wa pili wa Arsenal kutwaa tuzo hiyo ya kila mwezi katika kampeni hii, baada ya Martin Odegaard kuchaguliwa kuwa mchezaji bora katika kipindi cha Novemba na Desemba

Nae mlinda lango wa Arsenal Ramsdale ameshinda tuzo ya mlinda lango bora ya Ligi Kuu ya Uingereza mwezi Machi kwa mara ya kwanza, wakati Mikel Arteta akishinda tuzo ya Meneja bora

Arsenal imeshinda tuzo tatu kati ya nne zinazotolewa katika ligi kuu kila mwezi

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post