Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Horoya AC, yamekamilika
Robertinho amesema wachezaji wake wanatambua umuhimu wa mchezo huo ambao wanahitaji kushinda ili kutinga robo fainali
"Tunawaheshimu wapinzani wetu lakini tuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri mbele ya mashabiki wetu hapo kesho"
"Tulicheza vizuri mchezo wa kwanza lakini hatukutumia vyema nafasi tulizotengeneza lakini tumefanyia kazi mapungufu kuona tunafanya vizuri zaidi"
"Haikuwa rahisi kushinda mechi mbili dhidi ya Vipers Fc lakini wachezaji wetu walipambana, naamini siku ya kesho tutakuwa na wakati mzuri pia"
"Tunataka kucheza vizuri na kushinda, hii ni mechi kubwa tunapaswa kujitolea kwa ari kubwa, tunataka kushinda mchezo huu"
"Tunapaswa kucheza vyema tunapokuwa na mpira lakini pia hata pale bila ya mpira kwani tutakutana na nyakati zote hizi"
"Siwezi kuweka hadharani mbinu na kikosi nitakachotumia hapo kesho lakini nawahakikishia tuna timu imara, wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huu muhimu," alisema Robertinho
Nae nahodha msaidizi wa Simba Shomari Kapombe amesema wamekamilisha maandalizi kuelekea mchezo huo na wana matumaini kuwa watapata matokeo mazuri
"Tunajua mechi haitakuwa nyepesi, lakini pia tunajua hii ni mechi muhimu sio kwa Simba tu, bali kwa nchi hivyo wachezaji tuko tayari, muhimu tunawahitaji mashabiki wetu waje kwa wingi, tunawaahidi kupata ushindi," alisema Kapombe
Post a Comment