Rais wa zamani wa CAF, Ahmad Ahmad amemaliza kifungo chake na kuamua kutema nyongo kuhusu mahusiano ya CAF na FIFA akiyaita ya 'kibeberu' na sio ya kuusaidia mpira wa Afrika!
Ametoa kauli hiyo mara tu baada ya kumaliza kifungo chake cha miaka miwili alichokuwa anakitumikia kutokana na kufungiwa kujihusisha na masuala ya soka kwa sababu mbalimbali. Moja kati ya sababu ni matumizi mabaya ya ofisi yake akiwa Rais wa CAF.
Mwaka 2020 Kamati ya Maadili ya FIFA ilimfungia miaka mitano lakini Ahmad alikata rufaa kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa masuala ya Michezo CAS adhabu ikapunguzwa toka miaka mitano hadi miwili.
Sababu ya yeye kufungiwa anaiita ni sababu ya kisiasa kwenye mpira! Kwa sababu alitofautiana na Rais wa FIFA Gianni Infantino.
Walitofautiana nini? Infantino kwa kujua fika Bara la Afrika lina mtaji wa kura nyingi, ameamua kuliweka karibu.
Mkasa unarudi nyuma kidogo tangu Infantino aliposhinda kiti cha Urais wa FIFA mwaka 2016, moja ya ajenda zake ilikuwa ni kumuondoa madarakani aliyekuwa Rais wa CAF Mzee Issah Hayatou ambaye aliongoza kwa miaka 29.
Baada ya kufanikiwa kumtoa, Infantino alimwambia Ahmad Ahmad agombee Urais wa CAF! Ahmad akashinda uchaguzi na kuwa boss wa CAF.
Mikakati ya Infantino ilikuwa ni namna gani ataweza kuhudumu kwenye kiti cha Urais wa FIFA kwa muda mrefu, ndio maana akaliweka karibu Bara la Afrika kwa sababu lina mtaji mkubwa wa kura! Akaleta sera ya FIFA kuendesha baadhi ya maeneo ya CAF kimkakati ili kusaidia soka la Afrika kukua.
Akamleta mwanamama Fatma Samoura kwenye eneo la fedha na utawala [CAF] ili kusaidia uendeshaji wa shughuli za CAF.
Ahmad baada ya kupokea hiyo taarifa akawaruhusu kuingia kwenye mifumo ya CAF kufanya shughuli za Utawala na Fedha huku akiamini baada ya muda wataondoka wakiwa wamewaachia uzoefu watendaji wengine wa CAF.
Siku moja wakiwa kwenye kikao, Ahmad akamchana Infantino kwamba kwa sasa CAF inaweza kujiendesha kwa hiyo wale wataalam wanaweza kusepa! Kauli ile ilimkwaza Infantino akasusia kiao akaondoka bila kuaga moja kwa moja airport akasepa😄
Na hapo ndipo likaanzia anguko la Ahmad Ahmad, zikaanza kuzaliwa kesi juu ya utawala wake na makandokando! Mwisho wa siku akafungiwa.
Post a Comment