Rais Samia aongeza dau Sasa Kila BAO ni Milioni 10

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Awali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan aliahidi kuizawadia timu ya Taifa 'Taifa Stars' Tsh Milioni 500 kama itafanikiwa kufuzu fainali za michuano ya Afcon 2023 zitakazofanyika huko Ivory Coast


Jana baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uganda katika mchezo uliopigwa huko Misri, Rais Samia ameongeza bonas kwa Stars


Katika michezo mitatu iliyobaki, Stars itavuna Tsh Milioni 10 kwa kila bao watakalofunga


Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa amesema kuanzia mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda ambao utapigwa Jumanne, Tsh Milioni 10 zitaanza kutolewa kwa kila bao la Stars


Rais Samia anatoa Tsh Milioni 5 kwa timu za Simba na Yanga kwa kila bao wanalofunga kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho barani Afrika


Takribani Tsh Milioni 85 zimetolewa katika mechi tano za hatua ya makundi ambazo Simba na Yanga wamecheza mpaka sasa

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post