Nabi afunguka kinachoendelea kati yake na beki wa Yanga mpya Mamadou Doumbia


 Mashabiki wengi wa Yanga wana shauku ya kumuona mlinzi Mamadou Doumbia aliyesajiliwa kutoka klabu ya Stade De Malien ya Mali katika dirisha dogo la usajili


Tangu asajiliwe, Doumbia aliyekuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Mali iliyoshiriki michuano ya CHAN iliyofanyika Algeria, alicheza kwa takribani dakika 45 mchezo wa kombe la FA dhidi ya Rhino Rangers

Ratiba ya mechi za Leo jumamosi

Mara kadhaa kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alitoa ufafanuzi kwa nini Doumbia hapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza


"Nimeona watu wanaongelea sana kuhusu Mamadou, sio kila mchezaji akiletwa basi ataanza kucheza kwa haraka, huyu ni beki wa kati hili ni eneo ambalo unahitaji utulivu kumuingiza mtu mpya"


"Tunafanya kazi kubwa sasa ya kumfanya Mamadou anazoea falsafa ya soka letu, wakati wake ukifika atacheza tu akishafanikiwa kucheza kama tunavyotaka," alisema Nabi katika moja ya mahojiano yake


Ni changamoto kwa Nabi kufanya mabadiliko kwenye safu yake ya ulinzi hasa katika kipindi hiki ambacho mabeki wote wanafanya vizuri


Dickson Job, Yannick Bangala, Bakari Nondo Mwamnyeto na Ibrahim Bacca wote wanacheza vizuri huku wakiwa wameshazoeana


Haikuwa rahisi pia kwa mlinzi wa kushoto Joyce Lomalisa ambaye alihitaji kusubiri kabla ya kujihakikishia nafasi


Hata kwa Lomalisa wakati hapati nafasi ya kucheza, wengi waliponda usajili wake lakini sasa kauli hizo hazipo


Doumbia kukaa nje haimaanishi kuwa hana ubora kuwazidi wachezaji aliowakuta, bali ni utaratibu tu wa Nabi kuhakikisha mchezaji huyo anafahamu vyema falsafa ya Yanga na pia kuzoeana na wenzake

Je unatafuta Ajira tembelea tovuti hii Sasa Kwa matangazo yote ya kazi BOFYA HAPA SASA

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post