Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Klabu ya Simba imejihakikishia kuvuna Tsh Bilioni 1.5 kutoka kwa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) baada ya kufanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Juzi Simba ilitinga hatua hiyo kibabe kwa kuwafumua Horoya Ac mabao 7-0 katika moja ya vipigo vya kihistoria kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
Simba inakuwa timu ya pili kushusha 'kipigo heavy' katika michuano hiyo TP Mazembe ikishikilia rekodi ya ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Club Africain
CAF iliongeza zawadi za fedha ambazo timu zitalipwa kila hatua kuanzia makundi mpaka bingwa wa mashindano
Kama Simba itafanikiwa kutinga nusu fainali itavuna takribani Tsh Bilioni 2 wakati ikitinga fainali itakuwa na uhakika wa kuvuna Tsh Bilioni 2.9 na kama itwaa ubingwa basi mipesa itakuwa mingi zaidi kufikia Tsh Bilioni 5.8
Post a Comment